March 24, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kama Simba akishinda viporo vyake vyote saba ndio anaweza kukata tamaa ya ubingwa msimu huu lakini kwa sasa anawaona kama wanapiga makelele tu. Zahera anasema kupoteza dhidi ya Lipuli siyo ishu sana kwa vile bado mapambano yanaendelea.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 67 imecheza michezo 28, ikifuatiwa na Azam FC, wenye pointi 59 na michezo 28, wakati wapinzani wao Simba wakiwafukuza kwa mwendo kasi ambapo tayari wameshajikusanyia pointi 54 katika michezo 21 waliocheza hadi sasa.

Zahera ameliambia Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili kuwa; “Nitaanza kupoteza matumaini ya ubingwa baada ya kuiona Simba imeshinda viporo vyao vyote, kwani kama wakifanikiwa hivyo maana yake watakuwa wamekusanya pointi nyingi kuliko sisi au Azam, zaidi ya hapo sina shaka hata kidogo ya kuendelea kugombea ubingwa.”

“Kila mmoja anaijua changamoto yetu ya kiuchumi, hivyo hatujali sana hilo zaidi tunaangalia ubingwa ambao kwetu tukifanikiwa kuutwaa ninaimani utatufanya tupate hamasa kubwa ya kushiriki mashindano ya kimataifa tukiwa na nguvu nzuri.

“Mikakati iliyopo kwa sasa inaweza kufanikisha malengo mazuri ya usajili msimu ujao,” alisema Zahera ambaye ni Mkongomani mwenye uraia wa Ufaransa anayeishi Ufukwe wa Kawe Dar es Salaam.

3 COMMENTS:

  1. Kwa kuwa ulipata matokeo na sasa unafikiria kuwa mwenzako hatapata matokeo...Kabla labda ujiulize kama kuna sababu ya kumzuia simba kupata matokeo.HAIPO WEWE MJINGA!

    ReplyDelete
  2. Wewe unayemtukana zahera zahera kosa lake ni Nini? Acha kutafuta umaarufu kupotia blog za watu,ukitaka matus anzisha yako,Saleh jembe fyekelea mbali watu Kama Hawa wanaotaka kuifanya blog hi kuwa ya watu wahuni

    ReplyDelete
  3. Zahera ni mjinga na kama sio mjinga ni kichaa asiyetambua hali halisi!Ndiyo mana alitosa time yeke ilivyoenda Iringa eti kuisaidia AS Vita...matokeo yeke akapoteza kote!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic