RASHFORD KUTUA BARCELONA, OZIL, STERLING, MADRID: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO HIZI HAPA
Hizi hapa tetesi za soka barani ulaya leo Jumatano
Barcelona waanza kumnyatia Rashford
Barcelona wana nia kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza na Manchester United Marcus Rashford, 21. Mkataba wa mshambuliaji huyo na United utaisha 2020. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Barca wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 100 ili kumnasa Rashford. (Mirror)
Miamba hiyo ya La Liga inamouna Rashford kama mbadala wa muda mrefu kwa mshambuliaji wao nyota Luis Suarez, lakini United hawatazamiwi kumuuza mshambuliaji huyo. (ESPN)
United yaanza kumnyemelea beki Saliba
Manchester United wanamnyemelea beki kinda wa klabu ya St-Etienne William Saliba, 18. (Le 10 Sport - in French)
Arsenal kuwauza Ozil na Mkhitaryan
Arsenal wana nia ya kuwauza viungo wake Henrikh Mkhitaryan, 30, na Mesut Ozil, 30, kama njia ya kupunguza gharama kubwa za mishahara za klabu hiyo. (Mirror)
Real Madrid wamtaka Sterling
Real Madrid inapaswa kumsaini mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 24, badala ya kiungo wa Chelsea Eden Hazard, 28, anashauri kiungo wa zamani wa Blackburn Chris Sutton. (Mail)
Griezman achoshwa na tetesi za kuhama Atletico
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amesema kuwa "amechoshwa" na tetesi juu ya mustakabali wake. Mfaransa huyo mwenye miaka 28, amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa ikiwemo Barcelona na Manchester United. (Univision - in French)
Barcelona kumuuza Rakitic
Barcelona wanaweza wakamuuza kiungo Ivan Rakitic, 30, mwishoni mwa msimu huu huku Manchester United na Inter Milan wakitazamiwa kuwa watatupa karata zao ili kumnasa. (ESPN)
Liverpool kutumia pauni milioni 10 kwa Godfrey
Liverpool wanajipanga kulipa ada ya usajili ya pauni milioni 10 ili kumnasa beki wa Norwich City Ben Godfrey, 21. (Football Insider)
Casillas kumaliza maisha ya soka na Porto
Kipa mkongwe na raia Spain, Iker Casillas, 37, ameongeza mwaka mmoja zaidi kwenye mkataba wake na klabu ya Porto na kusema atamaliza maisha yake ya soka na klabu hiyo ya Ureno. (Sky Sports)
Arsenal na Juventus zaingia vitani kwa beki Benfica
Arsenal na Juventus ni miongoni mwa vilabu vilivyoonesha nia ya kumsaini beki wa kushoto wa Benfica Alejandro Grimaldo, 23, ambaye ni raia wa Uhispania. (Calcio Mercato)








0 COMMENTS:
Post a Comment