March 5, 2019

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema sababu kubwa iliyomfanya asimtumie nahodha wake kwenye mchezo dhidi ya Alliance ni za kiufundi kutokana na uhitaji wa mchezo wenyewe.

Ibrahim Ajibu mzee wa 'mi-assist' alianza benchi na alitumia dakika zote 90 kuwa kocha mchezaji kwani hakupata nafasi ya kuingia kuonyesha udambwiudambwi wake kwenye mchezo huo ambao Yanga ilishinda kwa bao 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba.

"Sikuanza kumtumia Ajibu kwenye mchezo wetu dhidi ya Alliance kutokana na sababu za kiufundi, nilitumia muda mwingi kuwatizama Alliance nikagundua kwamba ni wachezaji wepesi na wana spidi Uwanjani nikaona mchezo huo hautakuwa sawa kwa Ajibu.

"Uwezo wa Ajibu kwenda kwa kasi akiwa ndani ya Uwanja ni mdogo hivyo nikaona ni kheri aanze benchi asubiri kwanza wale wenye kasi waanze na tumefanikiwa kupata pointi tatu, hesabu zetu zimekamilika na tunaanza kupiga hesabu kwa ajili ya michezo yetu inayofuata," amesema Zahera.

Mguu wa kulia wa Ajibu umetoa assist 13 huku assist moja akitoa kwa kichwa na kumfanya awe na jumla ya assist 14 akiwakimbiza wachezaji wote bongo kwa assist.

3 COMMENTS:

  1. Kocha jaribu kupunguza media coverage watanzania ni wapotoshaji sana wanaweza wakazua uongo out of your words....Ndio kuna njia sahihi za kuhimiza michango lakini kuweka wazi katika media hizi....kwani maadui watataka kutumia mwanya huu kuwavuruga wakati ligi bado inaendelea....na ukawashusha morali wachezaji.....Hii ni mbinu ya maadui kutaka kuwavuruga Yanga....kwahiyo Kocha usiwape nafasi hii...kwa kuwashurutisha wanachama wa Yanga wachangie...au la sivyo unasema utaiacha timu.....kuna sababu kwanini zoezi lina muitikio mdogo mojawapo Yanga hawana uongozi wa kuchaguliwa....uchaguzi wao umeingiliwa na TFF na Serikali na baadhi ya wanachama wasio waaminifu wakitumiwa na maadui kwahiyo ndio maana michango haiendi kama kocha unavyotaka....lakini uchaguzi ukifanyika mambo yatabadilika....kwahiyo kocha Zahera inabidi ashauriwe kwa busara katika hili....asiwape nafasi maadui kwa kwenda kwenye media na kusema kama wanachama na mashabiki wa Yanga hawataitikia kuchanga kwamba yeye ataicha timu....hiki ni kipindi cha kutulia na kuhamasisha uchaguzi...wanachama na mashabiki wa Yanga wawe kitu kimoja!

    ReplyDelete
  2. Kushinda kwenyewe umeshinda kwa bahati

    ReplyDelete
  3. Zahera anapenda sana kujigamba na kujisifu kuwa ni kochaa namba moja na waliobaki wote hawana wanalolijuwa. Timu yake iliishinda alliance bao moja tena kwa shida akitumia kikosi cha kwanza. Simba iliishinda Allience kwa mbili huku Simba ikianzia kwa nusu nzima kikosi cha pili. Kocha wa simba hana tabia ya kujigamba na mechi zake zote hufunga mwanzomwanzo tena zote kwa mabao mawili na kuendelea na bila ya kujigamba na hajawahi kufanya vitisho vyovyote vya kuihama timu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic