March 27, 2019


Mtendaji Mkuu wa Simba SC Crescentius Magori amesema wanachama wa Simba wa Morogoro wamejitahidi kurekebisha sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Licha ya kujitahidi kumwagilia maji, bado sehemu zote za Uwanja hazijaota nyasi vizuri kutokana na jua kuwa kali zaidi ya walivyotarajia.

Hata hivyo Magori amesema watacheza hapo Jumapili na Mbao FC kwa sababu kwenye vita hawapaswi kuchagua silaha.

Kuhusu uwanja wa klabu ya Simba uliopo eneo la Bunju Dar es salaam, Magori amesema nyasi bandia zilikuwa zinashikiliwa na Takukuru kwa sababu ya uchunguzi uliokuwa unaendelea.

Lakini wanashukuru uchunguzi umeisha na nyasi zimeruhusiwa kutoka kwa hiyo wakati wowote ujenzi utaanza,na ujenzi ukianza ndani ya wiki mbili Simba itakuwa na uwanja wake wa kufanyia mazoezi.

CHANZO: SPORTS XTRA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic