March 24, 2019


KUELEKEA kwenye mchezo wa leo kati ya Taifa Stars na Uganda, utakaochezwa Uwanja wa Taifa saa 12:00 Jioni wataalamu wa masuala ya mpira wamezungumza na SpotiXtra juu ya nafasi ya Stars kwenye mchezo wa leo wamesema kama kama ifuatavyo:-

Seleman Matola, ambaye ni kocha wa timu ya Lipuli amesema kuwa mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi ya Uganda kwenye msimamo licha ya kufuzu kwani watatumia nguvu kubwa kujilinda na kushambulia siku ya leo.

"Wachezaji wana mzigo mzito ambao wamebebeshwa na mashabiki pamoja na Taifa kiujumla, nimeangalia namna hamasa ilivyo kubwa kila mmoja amejitoa kwa ajili ya mchezo wa leo, kazi ni kwa wachezaji kupambana kupata matokeo chanya uwanjani na mashabiki watoe dhana ya kuachiana kwenye mpira hiyo haipo duniani kote," amesema Matola.


Saleh Jembe, amesema kuwa kwa sasa ni zamu ya Stars kufufua matumaini ya kupenya Afcon ili kuwaokoa mashabiki ambao wamekuwa wakishabikia mataifa ya magharibi kutokana na kukosa wawakilishi kwa muda mrefu kutoka Tanzania.

"Kwa sasa ni sawa na kusema tonge lipo mdomoni, kuna kila namna ya kutaka kubadili upepo na historia isome tofauti. Wanaoweza kufanya hivyo ni mimi na wewe na huu ndio wakati wenyewe," amesema Jembe.

Boniface Pawasa ambaye ni kocha wa timu ya Taifa ya Beach Soccer, amesema kuwa ushindi unawategemea wachezaji kwani kazi ya mashabiki imekwisha kutokana na hamasa ambayo ipo hivyo ni muda tu utaamua namna gani mshindi atapatikana.

"Ushindi wa leo umeshikiliwa na wachezaji wenyewe kwa kuwa wao ndio watakaocheza, miguu yao itaamua ndani ya dakika tisini za mchezo wa leo ambao utakuwa mgumu," amesema Pawasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic