March 25, 2019


Tetesi za soka zilizteka vyombo mbalimbali na vikubwa Barani Ulaya leo Jumatatu

Bale akaribishwa tena Tottenham

Gareth Bale atakaribishwa tena kwa shangwe katika klabu ya Tottenham iwapo winga huyo raia wa Wales mwenye miaka 29 ataamua kuondoka katika klabu yake ya sasa Real Madrid na kurejea London, amesema beki wa Spurs Ben Davies. (Goal)

Keita afunguliwa milango ya kuondoka Liverpool

Liverpool wanatazamia kumruhusu kiungo Naby Keita, 24, kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu na watakubali kula hasara katika thamani ya mchezaji huyo raia wa Guinea. (Sun)

United, Arsenal na Tottenham zaingia vitani kwa Andersen

Klabu za Manchester United, Arsenal na Tottenham zinamnyemelea beki kinda raia wa Denmark anayechezea klabu ya Sampdoria ya Italia Joachim Andersen, 22. (CalcioMercato)

Barcelona yawafanyia umafia Liverpool kwa Ligt

Liverpool watamkosa beki wa kati raia wa Uholanzi anayecheza katika klabu ya Ajax Matthijs de Ligt wakati huu ambapo rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu yupo safarini kwenda kufanikisha makubaliano ya kumnasa mlinzi huyo mwenye miaka 19. (Sun)

Aribo atajwa kutua Arsenal

Arsenal wanapanga kumsajili kiungo wa klabu ya Charlton Athletic Joe Aribo, 22, mwishoni mwa msimu. (Mirror)

United kuvunja rekodi ya usajili kwa Maguire

Manchester United wametaarifiwa kuwa itawalazimu kuvunja rekodi ya usajili ili kumnasa mlinzi raia wa Uingereza Harry Maguire, 26, anayekipiga katika klabu ya Leicester. (Star)

Majogoo watimba Milan kusaka saini ya Skriniar

Liverpool wameingia katika kinyang'anyiro cha kumnyemelea beki wa Inter Milan na raia wa Slovakia Milan Skriniar, 24. (TeamTalk)

Varane kumfuata Ronaldo Juve

Juventus wanatarajiwa kumsaka beki wa Real Madrid Mfaransa Raphael Varane , 25, baada ya mlinzi huyo kuiambia klabu yake kuwa anataka kuihama. (Football Italia)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic