Tukiondoa siasa watanzania tunataka kiongozi wa aina gani kuliongoza taifa letu? Baada ya nchi yetu na wananchi wake kwa miaka mingi kuozea katika mfumo wa maisha wa kiujanja ujanja katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Baada ya miaka mingi nchi yetu na serikali zetu kutokuwa na watendaji waadilifu. Baada ya miaka mingi ya nchi yetu kupitia mamlaka husika kutothamini na kutotoa haki stahiki kwa watanzania wanaoifanyia makubwa nchi hii. Baada ya miaka mingi ya nchi yetu kuwa na mfumo wa kuwanufaisha wanasiasa peke yake, maana ilishafika wakati kwa nchi yetu wataalam wote wanaacha taaluma zao wanakimbilia kwenye siasa. Nchi ikeshakuwa kila mtu ni mwanasiasa kazi yake kuitisha mikutano na kupiga domo nani atafanya kazi? Ujio wa Magufuli umekuja ghafla kama kiongozi wa nchi kiasi kwamba wao wenyewe watanzania licha ya kumuomba Mwenyezi Mungu siku nyingi aweletee kiongozi atakaepambana na dhuluma nyingi zinazowatafuna watanzania lakini cha ajabu ni kwamba bado kuna baadhi ya watanzania wanaendelea kuota na kuburuzwa kimawazo na wanasiasa walaghai kiasi cha kushindwa kutambua haki yao ya msingi kuongozwa na kiongozi bora. Mwanasiasa mara nyingi huwa anaweka mbele maslahi yake binafsi na taasisi iliomsimamisha huku akijifanya kuwa anauchungu wa nchi. Kumjua mwanasiasa mnafiki, Mafano mzuri ni pale kama akitokea mwanafamilia mmoja kuugua ugonjwa kwa muda mrefu tu lakini kwa bahati nzuri akatokezea Daktari akawa anamtibu na afya ya mgonjwa ikaanza kuimarika likini ghafla kunajitokeza baadhi ya wanafamilia kuchukizwa na jitihada za Daktari zinazompelekea mgonjwa kupona sasa ni nani mchawi hapo? Nchi yetu Tanzania kwa miaka mingi kumekuwepo na sera ya kuwaweka pembeni na kutowajali wataalam wa fani mbali mbali kuiongoza nchi yetu na badala yake nafasi zao kubakwa na wanasisa na hii ilipelekea watu au watendaji wa taasisi mbali mbali nchini kuziongoza taasisi hizo kutokana na ushawishi wao kisiasa na sio uwezo wao kiutendaji na ufahamu wao katika dhamana husika. Muheshimiwa rahisi Magufuli ameondosha hilo na anaendelea kupambana na kuwajali wasomi na wataalamu wetu kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kuonesha uwezo wao katika kulitumikia taifa kwa faida na maslahi mapana ya nchi. Kama ilivyokuwa background ya maisha yake ya kazi ya Magufuli kuwa Mwanasayansi kitaaluma. Wanasayansi duniani kote huwa wanasifa ya kusimamia ukweli wa jambo katika uhalisia wake na mara nyingi wamekuwa na migogano ya mara kwa mara na wanasiasa. Kikubwa watanzania tunatakiwa kumuunga mkono kiongozi wetu wa nchi kwa nguvu zetu zote kwa zana kubwa ya kuliletea Taifa letu maendeleo na si kwa jambo jengine kwani wakati wetu amefika kama Taifa kutoboa na hayo ya wanasiasa wanaompinga jemedari wa mapambano huku tukielekea kushinda vita tunatakiwa kuwaachia wanasiasa wenyewe lakini kabla ya kuwaunga mkono wanasiasa wanaompinga Magufuli kama watanzania twenye ufahamu wetu kamili sio wakupelekeshwa,tungewataka hawa wanasiasa kuyatambua,kuthamini na kuunga mkono kiroho safi hizi jitihada za serikali ya awamu ya tano za kuwaletea watanzania maendeleo kwa sababu jitihada si za Magufuli peke yake jitihada hizi ni watanzania waliowengi,kuna wanamichezo,madatakari, marubani wa ndege,wanajeshi, mainjinia nakadhalika nakadhalika. Na kama kuna mwanasiasa ana chembe ya kigugumizi cha kuunga mkono jitihada zinazoendelea na amejikita katika kubeza tu basi tujue mtu huyo ni dui wa maendeleo yetu kama Taifa na hatutakiwi kumchekea hata kidogo.
Tukiondoa siasa watanzania tunataka kiongozi wa aina gani kuliongoza taifa letu? Baada ya nchi yetu na wananchi wake kwa miaka mingi kuozea katika mfumo wa maisha wa kiujanja ujanja katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Baada ya miaka mingi nchi yetu na serikali zetu kutokuwa na watendaji waadilifu. Baada ya miaka mingi ya nchi yetu kupitia mamlaka husika kutothamini na kutotoa haki stahiki kwa watanzania wanaoifanyia makubwa nchi hii. Baada ya miaka mingi ya nchi yetu kuwa na mfumo wa kuwanufaisha wanasiasa peke yake, maana ilishafika wakati kwa nchi yetu wataalam wote wanaacha taaluma zao wanakimbilia kwenye siasa. Nchi ikeshakuwa kila mtu ni mwanasiasa kazi yake kuitisha mikutano na kupiga domo nani atafanya kazi?
ReplyDeleteUjio wa Magufuli umekuja ghafla kama kiongozi wa nchi kiasi kwamba wao wenyewe watanzania licha ya kumuomba Mwenyezi Mungu siku nyingi aweletee kiongozi atakaepambana na dhuluma nyingi zinazowatafuna watanzania lakini cha ajabu ni kwamba bado kuna baadhi ya watanzania wanaendelea kuota na kuburuzwa kimawazo na wanasiasa walaghai kiasi cha kushindwa kutambua haki yao ya msingi kuongozwa na kiongozi bora. Mwanasiasa mara nyingi huwa anaweka mbele maslahi yake binafsi na taasisi iliomsimamisha huku akijifanya kuwa anauchungu wa nchi. Kumjua mwanasiasa mnafiki, Mafano mzuri ni pale kama akitokea mwanafamilia mmoja kuugua ugonjwa kwa muda mrefu tu lakini kwa bahati nzuri akatokezea Daktari akawa anamtibu na afya ya mgonjwa ikaanza kuimarika likini ghafla kunajitokeza baadhi ya wanafamilia kuchukizwa na jitihada za Daktari zinazompelekea mgonjwa kupona sasa ni nani mchawi hapo? Nchi yetu Tanzania kwa miaka mingi kumekuwepo na sera ya kuwaweka pembeni na kutowajali wataalam wa fani mbali mbali kuiongoza nchi yetu na badala yake nafasi zao kubakwa na wanasisa na hii ilipelekea watu au watendaji wa taasisi mbali mbali nchini kuziongoza taasisi hizo kutokana na ushawishi wao kisiasa na sio uwezo wao kiutendaji na ufahamu wao katika dhamana husika. Muheshimiwa rahisi Magufuli ameondosha hilo na anaendelea kupambana na kuwajali wasomi na wataalamu wetu kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kuonesha uwezo wao katika kulitumikia taifa kwa faida na maslahi mapana ya nchi. Kama ilivyokuwa background ya maisha yake ya kazi ya Magufuli kuwa Mwanasayansi kitaaluma. Wanasayansi duniani kote huwa wanasifa ya kusimamia ukweli wa jambo katika uhalisia wake na mara nyingi wamekuwa na migogano ya mara kwa mara na wanasiasa. Kikubwa watanzania tunatakiwa kumuunga mkono kiongozi wetu wa nchi kwa nguvu zetu zote kwa zana kubwa ya kuliletea Taifa letu maendeleo na si kwa jambo jengine kwani wakati wetu amefika kama Taifa kutoboa na hayo ya wanasiasa wanaompinga jemedari wa mapambano huku tukielekea kushinda vita tunatakiwa kuwaachia wanasiasa wenyewe lakini kabla ya kuwaunga mkono wanasiasa wanaompinga Magufuli kama watanzania twenye ufahamu wetu kamili sio wakupelekeshwa,tungewataka hawa wanasiasa kuyatambua,kuthamini na kuunga mkono kiroho safi hizi jitihada za serikali ya awamu ya tano za kuwaletea watanzania maendeleo kwa sababu jitihada si za Magufuli peke yake jitihada hizi ni watanzania waliowengi,kuna wanamichezo,madatakari, marubani wa ndege,wanajeshi, mainjinia nakadhalika nakadhalika. Na kama kuna mwanasiasa ana chembe ya kigugumizi cha kuunga mkono jitihada zinazoendelea na amejikita katika kubeza tu basi tujue mtu huyo ni dui wa maendeleo yetu kama Taifa
na hatutakiwi kumchekea hata kidogo.
hayo ni maoni na mtazamo wako
ReplyDeleteNi mtizamo uliojaa uhalisia wa mambo na zidumu fikra za Magufuli, Taifa stars oyee.
ReplyDelete