WAWA AMTAJA ANAYEMPA JEURI YA KUWAUA MAZEMBE DAR
BEKI kisiki wa Simba, Paschal Wawa amesisitiza kuwa hawana hofu hata kidogo dhidi ya TP Mazembe ambayo wanacheza nayo kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika April 5 Uwanja wa Taifa.
Wawa amesema; “Nina imani kurejea kwa Erasto Nyoni ndani ya timu kunaongeza morali ya kushindana kwani nafurahi sana sapoti yake na namna anavyofanya akiwa Uwanjani ni kitu cha kujivunia.
“Furaha yangu ni kuona timu inapata matokeo chanya kwenye mechi zote ambazo tunacheza hapo.
"Kikubwa ni kuomba kuwa na afya bora na Mungu azidi kutulinda hali itakayotufanya tupate matokeo chanya hatuna hofu na hao Mazembe,” alisema Wawa ambaye mtaani wanamtania kama Sultani.








Unaongea Sana kuliko vitendo pia unaongoza kwa kutoa maboko jirekebishe
ReplyDelete