March 26, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umeingiwa na hofu juu ya watani zao wa jadi Simba kutokana na kushinda mechi zao za viporo mpaka sasa.

Kutokana na hofu hiyo, Kocha wake Msaidizi, Noel Mwandila, amewaombea dua na sala Simba ya kuwaona wakipoteza mechi zao zijazo ili waweze kuwapa nafuu.

Ikumbukwe katika msimamo wa Ligi Kuu Bara hivi sasa Yanga imeiacha Simba kwa alama13 ikiwa na pointi 67 kileleni huku Simba walio nafasi ya tatu wakiwa na 54.

Noel ameeleza kuwa kuwa kila mmoja hivi sasa anatamani kushinda mechi zake lakini akisema kupoteza kwa Simba kutawapa unafuu zaidi.

"Najua kila mmoja anamwombea mwenzake mabaya, lakini Simba kama wakipoteza itakuwa vizuri zaidi." alisema.

Mpaka wekundu hao wa Msimbazi wameshikilia nafasi hiyo ya tatu wakiwa na michezo 7 mkononi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic