KIKOSI cha Azam FC jana kilianza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Aprili 14 Uwanja wa Sokoine.
Wachezaji wa Azam FC walipewa mapumziko ya siku moja baada ya mchezo wa Mbao FC uliochezwa Uwanja wa Nyamagana uliokamilika kwa suluhu.
Azam FC watashuka Mbeya wakiwa na kumbukumbu ya kuonja joto ya jiwe baada ya kupoteza mchezo wao uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine kwa kuchapwa na Prisons bao 1-0.
Kwenye msimamo wa ligi Azam FC wapo nafasi ya pili wakiwa wamecheza michezo 30 kibindoni wana pointi 63 na Mbeya City wao wana pointi 31 kibindoni wana pointi 40 nafasi ya 9.
Asante kwa habar motomoto
ReplyDelete