BAADA ya Simba kupoteza nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya nusu fainali, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema nguvu zake kubwa anaziwekeza kwenye ligi.
Simba ilipoteza mchezo wake wa pili mbele ya TP Mazembe kwa kufungwa mabao 4-1 hali iliyofanya ndoto yao ya kusonga mbele kuishia Congo.
Aussems amesema kuwa amejifunza mengi na kugundua kwamba kikosi chake kina uwezo mkubwa hivyo makosa aliyofanya atayafanyia kazi ila kwa sasa nguvu ni kwenye ligi.
"Tumepoteza nafasi yetu ya kusonga mbele ila hakuna cha kujutia sana kwa kuwa ushindani ulikuwa mkubwa nasi tumepambana, haikuwa bahati yetu sasa tunaweka akili yetu kwenye ligi.
"Tuna michezo mingi ya kucheza na wachezaji tayari wameshaanza kuona namna ushindani ulivyo na mashindano ya kimataifa yanavyokwenda nina amini msimu ujao tutakuwa na nafasi nzuri zaidi tukirejea," amesema Aussems.
Kikosi cha Simba leo tayari kimefika salama jijini Tanga na jioni kitaanza mazoezi kujiandaa kuwakabili Coastal Union siku ya Jumatano.








0 COMMENTS:
Post a Comment