April 19, 2019


SIMBA ipo katika kipindi kigumu cha ratiba ya Ligi Kuu Bara, hiyo ni kutokana na kutakiwa kucheza mechi tano ndani ya siku kumi, ambapo kutokana na hali hiyo, takwimu zinaonyesha kuwa wakishinda mechi hizo zote watajiweka katika mazingira mazuri ya kubeba ubingwa.

Timu hiyo itacheza mechi hizo tano mfululizo kuanzia wikiendi hii, ikiwa ni baada ya kuifunga Coastal Union mabao 2-1, juzi Jumatano.

Simba ambayo ina pointi 60 kwa sasa, ina’ viporo’ tisa ili wafikie idadi sawa na mechi za Yanga ambao wamecheza mechi 32 na wanaongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 74.

Katibu Mkuu wa Simba, Dk. Anold Kashembe, amesema kocha wao pamoja na wachezaji wanatambua ugumu wa ratiba hiyo, hivyo wamejipanga kwenda kupambana katika mechi zote. 

“Ratiba hii tumekubaliana nayo, kocha pamoja na wachezaji wameikubali, ni lazima tupambane. Mipango yetu tulishajadiliana kuwa ni vijana na kocha wakapambane na tuweze kuondoka na matokeo kwenye mechi hizo na kutetea ubingwa wetu tena.

 “Ratiba hii tulishirikishwa na bodi ya ligi, kwa jinsi hali ilivyo haikwepeki hata kidogo, kupambana ndiyo jambo la msingi,” amesema. 

Mechi za Simba ndani ya siku 10 hizi hapa

Aprili 20 vs Kagera (Kaitaba)

Aprili 23 vs Alliance (Kirumba)

Aprili 25 vs KMC (Kirumba)

Aprili 27 vs Biashara (Karume)

Aprili 30 vs JKT (Taifa)

Kutoka Championi

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic