April 6, 2019


Winga wa timu ya Yanga, Deus Kaseke, amesema kuwa walistahili kushinda mchezo wao wa juzi dhidi ya Ndanda.

Yanga ililazimishwa sare ya 1-1 kwenye Uwanaja wa Nangwanda Sijaona katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa mjini Mtwara.

Kutokana na matokeo kuwa hivyo, Kaseke amesema walijitahidi kucheza mpira na walimiliki kwa asilimia nyingi lakini bahati haikuwa yao.

Amefunguka kuwa Ndanda walikuwa kama na bahati na akisema matokeo huwa yanakuwa ya aina tatu ikiwemo ni kushinda, sare na kufungwa.

Mbali na kutoa sare, Kaseke anaamini kuwa sare hiyo itasababisha kuzidi kupunguza nguvu za kupigania ubingwa ambao unawaniwa pia na watani zao wa jadi, Simba.

3 COMMENTS:

  1. Kuna kipindi Simba iliteleza kama katika mechi kadhaa hapo awali Yanga waliibeza sana Simba kuwa wazee wa kikosi kipana kisichokuwa na maana. Hapa nitaeleza tofauti ya matatizo ya Yanga na mafanikio ya Simba msimu huu wa ligi.
    (1) Tatizo moja kubwa la Yanga hivi sasa ni wachezaji kuchoka kiakili na kimwili na hapa Simba licha ya kukabiliwa na mashindano makubwa ya Africa lakini bado inatesa kwenye ligi pia, hii ni kutokana na upana wa kikosi chao kinachoweza kuwapa day off wachezaji na kuwa na muda wa kupumzika. Yanga kwa jinsi walvyoianza ligi ni lazima wangefikia mahala wangekwama tu kwani ligi ni ndefu ilihitaji timu yenye pumzi kubwa za mali na hali si ajabu Azam ndie atakae kuja kuwa mkaribu wa Simba kunako ubingwa.
    (2)Changamoto wanaoipata wachezaji wa Simba kwenye mechi za klabu bingwa Africa ni uzoefu tosha unaowajenga kujiamini zaidi wanapokutana na timu za nyumbani. Utaona Simba ya sasa pressing yao ya kutafuta goli inapokutana na tumu za ligi kuu huwa si za kawaida yaani pressure kama si goli watasababisha penalt.
    (3) Uongozi, Simba ina full nondo kwenye safu yake ya uongozi lakini Yanga kuna care givers wa kujitolea. Katika hali hii sio rahisi Yanga kushindana na Simba kunako uhalisia. Yanga waiombee Simba ibakie huko huko kwenye klabu bingwa Africa kwani kunaifichia Yanga udhaifu wake kwenye ligi kuu. Mfano Simba angerudi mapema kwenye ligi kuu na kula viporo vyake vyote kwa mafanikio basi jangwani kungekuwa hali tete hivi sasa yaani kiuhakika kabisa amani ya Yanga hivi sasa au msimu huu wa ligi inategemeana na uwezo wa Simba kubakia kwenye klabu bingwa Africa. Yanga wala hawana haja ya kuhofia au kuhoji viporo cha Simba la msingi wamuombee Simba afike mbali zaidi Africa kutakuwa na manufaa mapana zaidi kwa Yanga kitaifa na kimataifa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic