April 16, 2019


KIKOSI cha Yanga kesho kitakuwa Morogoro Uwanja wa Jamhuri kucheza mechi ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar huku wakiwa na majembe mapya mawili ambayo yalikuwa nje kwa muda.


Ibrahim Ajibu ambaye ni nahodha alikosa michezo minne ya Yanga kutokana na kusumbuliwa na majeraha huku Abdalah Shaibu Ninja akimaliza adhabu yake baada ya kufungiwa mechi tatu.

Wachezaji hao wawili wamempa faraja kocha mkuu, Mwinyi Zahera ambaye anaamini wataziba pengo la beki kisiki Kelvin Yondan mwenye kadi nyekundu na Feisal Salum 'Feitoto' mwenye kadi ya tatu ya njano.

Zahera amesema Ratiba kwetu ni ngumu kwani tumecheza na Ndanda kisha tukaifuata Lyon na Kagera Sugar na sasa ni zamu ya Mtibwa Sugar, mashabiki watupe sapoti kwani nina kikosi kipana.


1 COMMENTS:

  1. Mbona jana mliandika Ajib amezingua tena kuungana na timu kuelekea Morogoro?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic