RATIBA MECHI YA YANGA YAPANGULIWA
Mratibu wa klabu ya Yanga Hafidh Saleh amethibitisha kuwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar uliotakiwa kupigwa majira ya saa 10 Jioni umerudishwa nyuma kwa masaa mawili na sasa utapigwa majira ya saa 8:00 mchana. .
Mchezo huo umerudishwa nyuma ili kupisha mchezo wa AFCON U17 kati ya Serengeti Boys dhidi ya Uganda utakaopigwa majira ya saa 10 Jioni.
Kikosi cha Yanga kimezidi kujifua mjini Morogoro kuelekea mechi hiyo kikiwa na hasira ya kuurejesha ubingwa wake.
Ikumbukwe Yanga ndiyo mabingwa wa kihitostoria baada ya kuchukua taji la ligi kuu mara 27 na Simba wakichukua mara 18








0 COMMENTS:
Post a Comment