April 1, 2019


UONGOZI wa Simba umejipanga kwelikweli kuelekea mchezo na TP Mazembe lakini kwanza wanataka kuipiga Mbao Jumapili mkoani Morogoro.

Simba na TP Mazembe zinakutana Aprili 6, mwaka huu jijini Dar es Salaam na watarudiana Aprili 13, mjini Lubumbashi DR Congo.

Katibu wa timu hiyo, Dk Anold Kashembe alisema; “Kama viongozi wa sekretarieti, tulikutana juzi Jumanne na kuweka mikakati yetu kama timu na Jumatano (jana) tutakutana wote pamoja na benchi la ufundi kuweza kuweka mambo sawa.

“Ila malengo yetu ni kufanya vizuri ndani na nje ili kuweza kusonga mbele katika hatua inayofuata na suala la kuwaangalia zaidi wapinzani wetu tutaanza kudili nalo baada ya mchezo wa Mbao na hata ule wa Aprili 6, ukipita ndiyo tutaanza utaratibu mwingine wa kushughulikia suala watu kwenda Lubumbashi.”

Kwa upande wa Kocha wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems alisema mbali na kuzungumza na Kocha wa As Vita Club, Florent Ibenge na kocha wa CS Constantine ambao ni marafiki za kuhusiana na wapinzani wake Mazembe.

DIDA Baada ya kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kuumia juzi katika mazoezi ataukosa mchezo na Mbao FC huku Deogratius Munishi ‘Dida’ akipewa jukumu hilo la Manula na timu ikiondoka kesho Ijumaa kwenda Morogoro.

Manula ambaye kwa sasa ni majeruhi amepewa mapumziko ya kutodaka na hata katika mazoezi ya jana Jumatano hakuweza kufanya mazoezi yale ya makipa badala yake alifanya ya kawaida na wachezaji wa ndani.

Kocha Patrick Aussem alisema; “Dida nimempa kazi ya Mbao FC siku ya Jumapili Aishi ataendelea kupumzika kutokana na majeruhi na hivyo atasaidiana na Ally Sali nitaenda kumuomba kule.”

“Pia leo (jana) wachezaji wengi hawakuwepo kwenye mazoezi hivyo Alhamisi (leo) watakuwepo wote kama Kagere na Zana walifika leo alfajiri na wengi wataingia hapa na kesho tutakuwa pamoja,”alisema Mbelgiji.

1 COMMENTS:

  1. ndugu mwandishi unazingua sana.. hii ni habari ya lini na leo ni lini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic