April 18, 2019


MOHAMED Mkopi wa Ndanda FC alipachika bao dakika ya 62 lililomshinda mlinda mlango wa Azam FC, limevunja mwiko wa kocha Idd Cheche kutopoteza baada ya kupokea mikoba kwa muda kutoka kwa Hans Pluijm.

Bao hilo pia limelipa kisasi cha Ndanda baada ya mchezo wa kwanza wa ligi kuu ulochezwa Uwanja wa Chamazi wakati timu ikiwa chini ya mholanzi Pluijm waliacha pointi zote tatu na walichapwa mabao 3-0.

Leo kikosi cha Azam kinaacha pointi tatu zote muhimu Uwanja wa Nangwada Sijona, Mtwara.


Cheche ameiongoza Azam kushinda mbele ya Lyon alishinda 3-1, JKT alishinda mabao 6-1, Singida United mabao 4-0, Kagera Sugar alishinda mabao 2-0, Mbao 0-0 na mchezo wa mwisho alishinda mbele ya Mbeya City kwa bao 1-0 kabla ya leo kupoteza mbele ya Ndanda.
Kwa sasa Azam imecheza jumla ya michezo 32 ikiwa na pointi 66 nafasi ya pili.

1 COMMENTS:

  1. Cheche umeanza nyodo siku nyingi ulionyesha dharau kwa kocha super aliyekuwa na mafanikio makubwa Yanga leo on a kinachoanza kukutokea na bado miele yak yupo YANGA tutakunyoosha vizuri goli 2-0 na waajiri wako wakufyekelee mbali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic