April 18, 2019


MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amenogesha vita ya mbio za kuwania kiatu bora cha ufungaji baada ya jana kufunga mabao mawili dhidi ya Coastal Union na kufikisha 16 ndani ya ligi.

Kagere sasa yupo sambamba na mkali wa kutupia Salim Aiyee wa Mwadui ambaye naye pia akaunti yake ina mabao 16.

Mshambuliaji kinara kwa upande wa Yanga ni Heritier Makambo ambaye ametupia mabao 15 mpaka sasa.

Msimu uliopita mpachika mabao bora alikuwa ni Emmanuel Okwi ambaye alifunga mabao 20 na msimu huu ametupia mabao 7 mpaka sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic