April 20, 2019


Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo imetangaza kuwa aliyekuwa Rais wake Moise Katumbi amerejea katika nafasi yake ya urais wa klabu.

taarifa imeeleza kuwa Katumbi amerejea katika klabu hiyo hiyo baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka kadhaa akikimbia adhabu ya kifungo kwa sababu za kisiasa.

Rais mpya wa DR Congo Felix Tshisekedi ambaye amekuwa akihudhuria mechiza Mazembe ikiwemo ya TP Mazembe na Simba, ametangaza maridhiano ya kisiasa na makundi mbali mbali nchini humo na adhabu ya kifungo cha Katumbi imetenguliwa.

Ujio wa Katumbi nchini humo umeleta chachu kubwa ndani ya klabu hiyo ambayo hivi sasa imetinga kucheza hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic