April 19, 2019


BEKI Mkongwe wa Simba, Erasto Nyoni amesema kuwa kilichowabeba kushinda mbele ya Coastal Union ni uzoefu wa ligi kama isingekuwa hivyo wangepoteza mchezo huo kwa kuziacha pointi tatu mkoani Tanga mbele ya Coastal Union kwani ilikuwa ni 'Mbinde' kuivunja ngome ya wapinzani wao.

Mchezo wa Coastal Union na Simba uliochezwa Jumatano Uwanja wa Mkwakwani ulikuwa ni wa kasi na Coastal Union walianza kupachika bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Raizin Hafidh dakika ya kwanza huku yale ya Simba yakifungwa kipindi cha pili na Meddie Kagere.

Nyoni amesema kuwa Coastal Union walikuwa kwenye ubora wao na walianza kwa kasi kushambulia na kulinda kwa wakati mmoja hali iliyoleta ushindani mkubwa.

"Kama sio kutumia uzoefu kwenye mchezo wetu dhidi ya Coastal Union mambo yalikuwa magumu, kwa sasa ni kama tumeanza ligi kwa sababu vita iliyopo mbele yetu ni kubwa zaidi ya tulikotoka na tumejipanga kwa ajili ya timu zote zinazokuja mbele yetu," amesema Nyoni.

Simba imetia timu Bukoba leo kwa ajili ya mchezo wao utakaochezwa kesho dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa uwanja wa Kaitaba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic