April 16, 2019


KIKOSI Cha Mbao FC kilicho chini ya kocha Salum Mayanga kwa sasa kinaivutia kasi Ndanda FC ya Mtwara kwenye mchezo wao wa ligi. 

michezo mitatu ya awali ya Mayanga ilikuwa dhidi ya Simba na alipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 kisha mchezo wake wa pili ulikuwa dhidi ya Biashara United alipoteza kwa kufungwa bao 1-0 kabla ya kutoka suluhu na Azam FC Uwanja wa CCM Kirumba.
 
Kituo kinachofuata kwa Mbao FC ni uwanja wao wa nyumbani CCM kirumba na watamenyana na Ndanda, FC Mei 05 mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni.

Mshambuliaji wa Mbao FC, Evarigestus Mujahukwi amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo hasa ukizingatia watakuwa nyumbani hawana cha kupoteza.

Mbao FC imecheza michezo 34 imejikusanyia pointi 40 ikiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic