SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepangua ratiba ya mechi za leo Jumatano za Ligi Kuu Bara ambapo Simba itacheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga na Yanga itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mechi hizo awali zilipangwa kuchezwa kuanzia saa 10:00 Jioni lakini sasa zote zitaanza saa 8:00 mchana kutokana na kupisha mechi ya Serengeti Boys dhidi ya Uganda ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Vijana chini ya miaka 17.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Boniface Wambura amesema kuwa mechi hizi zote zitachezwa leo saa 8:00 mchana badala ya saa 10:00 Jioni kama ilivyokuwa awali.
"Kutokana na hali ya Serengeti Boys kucheza leo saa 11:00 Jioni tumelazimika kubadilisha muda wa mechi za ligi ili kupisha mchezo wa Serengeti na timu tayari zimepewa taarifa," amesema








Hao TFF ni waganywa wa akili. Hizo mechi za Yanga na Simba zinachezwa mamia ya kilomita away from Dar zingeathiri kitu gani mechi ya Serengeti boys?
ReplyDelete