WAKATI leo Mabingwa watetezi Simba wakitarajiwa kumenyana na Coastal Union, saa nane kamili mchana Uwanja wa Mkwakwani itawakosa mabeki wake watatu tegemeo kutokana na kuwa majeruhi.
Simba itashuka kwa mara ya kwanza msimu huu kupambana na Coastal Union ambao wamerejea ligi kuu baada ya kushuka msimu wa mwaka 2015/16.
Wachezaji hao watakosekana kutokana na kupata majeraha walipokuwa wakivaana na TP Mazembe Lubumbashi, DR Congo isipokuwa Pascal Wawa aliumia kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kwenye mchezo wa leo James Kotei, Juuko Murshid na Pascal Wawa hawatakuwa sehemu ya mchezo kwa sababu walipata majeraha tukiwa Lubumbashi katika mchezo uliopita.
"Maandalizi yetu yanaendela ingawa bado wachezaji hawako fiti kivile kutokana na safari na tumetoka kucheza mechi ngumu lakini tunapambana kuona kila kitu kinakwenda sawa na kuona tunaondoka na pointi tatu," amesema Meneja.
Kutoka Championi







0 COMMENTS:
Post a Comment