April 19, 2019


OSCAR Mirambo, Kocha Mkuu wa Serengeti Boys amesema kuwa kesho watapambana ili kufuta makosa yote waliyoyafanya kwenye mechi mbili za nyuma kwenye michuano ya Afcon.
Serengeti Boys kwenye michuano ya Afcon kwa vijana chini ya miaka 17 walianza vibaya kwa kupokea kichapo cha mabao 5-4 mbele ya Nigeria na wakakubali kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Uganda.
Mirambo amesema matokeo mabaya wanayoyapata yanawaumiza ila hawajapanga itokee hivyo.
"Kupoteza michezo yetu iliyopita hatujapanga na tunapata maumivu makubwa kuona inatokea hali ya namna hiyo, kwa namna kundi lilivyo bado tuna nafasi ya kufuzu endapo tutashinda.
"Morali ya wachezaji ni kubwa na mbinu mpya ambazo tumewapa wachezaji zitawasaidia kupata matokeo ninawaomba mashabiki na watanzania wajitokeze, bado kundi letu lipo wazi," amesema Mirambo.
Serengeti Boys wanashikilia mkia kwenye kundi A lenye timu nne baada ya kucheza michezo miwili bila kupata pointi, kinara ni Nigeria ambaye tayari amekata tiketi ya kushiriki kombe la Dunia nchini Brazil.

2 COMMENTS:

  1. Watanzania sisi bado ni watu wa masihara sana mpira kocha bwana.Uzalendo sawa lakini kuna level fulani ya mashindano lazima tukubali kuwa bado hatuna wazawa wenye uwezo wa ukocha ambao wana uwezo wa kushindana na makocha wa kigeni.wakati fulani kulikuwa na malumbano kama kocha wa Serengeti boys abadilishwe kuelekea Afcon au la?watu wakan'gaka sana sana kwamba asibadailishwe na zaidi kwa sababu ya hoja ya tiketi ya kocha mzawa? Pengine ukienda deep yaani ukichimba zaidi kuhusiana na kocha huyo mzawa wa Serengeti boys yupo pale Kwa maslahi ya baadhi ya watu fulani nje na maendeleo ya vijana wetu na akija mgeni atatibua dili. Kwa wenzetu Under17 ndiko kwenye uwekezaji mkubwa zaidi wa wanataaluma wa mpira kwa upande wa makocha kwa sababu hapa kama ni lugha ya kiswahili ndipo tunaposema kambare mkunje bado mbichi kwani unaweza kumkunja kwa jinsi unavyotaka awe.Hapa panahitaji watu au mtu makini,fundi mwenye utaalamu uliobobea na aliekwisha pata majaribu na mafanikio kadhaa wa kadhaa katika kazi yake na sio mtu wa kujaribu. Wachezaji wengi wa kiafrica unaowaona wanacheza ulaya wameibuliwa au kuonekana kupitia under 17 ndio maana wenzetu hawana masihara hata kidogo kwenye haya mashindano.Klabu nyingi za kigeni hasa za ulaya huangaza wachezaji wa kuwasajili katika level hii labda kwa lengo lile la kutafuta kambare bado angali mbichi. kwa kiasi fulani ni aibu kwa Taifa. Nguvu nyingi zimetumika kuandaa Afcon ya vijana lakini hatuna timu ya kushindana katika mashindano hayo. Nina wasi wasi mkubwa yakwamba kinachotokea kwa Serengeti boys ndicho kitakachotokea kwa Taifa stars kule Misri.Lakini la kusikitisha ni kwamba viongozi wetu wengi wa taasisi za umma hawajamuelewa Magufuli bado na kunako michezo viongozi wake vichwa vyao ndio vumeoza kabisa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic