April 19, 2019


Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameliomba Shirikisho la Soka nchini TFF kumchukulia hatua za kinidhamu Kocha mkuu wa klabu Yanga, Mwinyi Zahera.

Kauli ya Manara imekuja kutokana na baadhi ya kauli zake za kulishutumu Shirikisho hilo na Bodi ya Ligi mara kwa mara juu ya Simba.

Manara amesema kuwa, Zahera amekuwa mara nyingi akiilalamikia bodi hiyo kuitengenezea mazingira Simba ya kuchukua ubingwa wa ligi.

Aidha ameeleza kuwa Zahera amekuwa hana heshima na mpira wa miguu yeye akifungwa anaishutumu TFF, Bodi ya Ligi, Marefa na klabu ya Simba.

6 COMMENTS:

  1. Amesahau alivyokuwa anacheza mechi mfululizo ktk uwanja wa taifa na kushinda....mbona simba walikaa kimya...akomae na viwanja vya mikoani...aache kulalamika na visingizio ili wanayanga wamuone kaonewa...uwezo tu hapo

    ReplyDelete
  2. Manara atakuwa na tatizo la Kisaikolojia kwa sababu kila siku anatoa matamko mabaya juu ya Yanga wakat TFF na Waamuzi wake ndio wanaweka mpango mkakati wa kuidhoofisha Yanga, hali inayotia hasira kwa watu wanaopenda mchezo wa soka nchini

    ReplyDelete
  3. Haji Manara ni msemaji asiye na mipaka ya kazi yake....aache kuleta chokochoko na chuki

    ReplyDelete
  4. Chokochoko na chuki analeta Zahera. Kushutumu timu bila ushahidi inaruhusiwa?
    Kwani ni uongo refa hakupigwa Mbeya mechi dhidi ya Prisons?Hakuna yaliypotokea Morogoro?
    Azam wachezaji wao walimzonga mwamuzi adhabu ikaja mara moja.Kufungiwa mechi 3 kwa wachezaji watatu nä faini.
    Kwanini kwa Yanga TFF inapata kigugumizi?
    Al ulikuwa mmojawapo wa wachangiaji wenye heshima katika blogu hii lakini na wewe siku za karibuni umekuwa shabiki maandazi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic