April 1, 2019



MLINDA mlango ambaye juzi aliibeba Yanga na kutimiza majukumu yake kwa kuipeleka hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho, Klaus Kindoki amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa hatua aliyofikia kwa sasa.

Kindoki aliokoa penalti mbili kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Alliance FC uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba hali iliyofanya Yanga kutinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa penalti 4-3 ambapo itakutana na Lipuli ya Iringa Uwanja wa Samora mwezi huu.

"Hatua nzuri ambayo nimefikia kwa sasa, ninamshukuru Mungu kwa kunipa nguvu na uvumilivu hasa katika kipindi kigumu ambacho nimepitia ila yote ni kheri kwangu kwani ni furaha kubwa sana hapa Yanga.

"Mashabiki ni watu muhimu kwangu nawashukuru kwa sapoti yao  na kunipa muda wa kufanya mengi zaidi, ninawaahidi kufanya mengi makubwa wazidi kunipa sapoti," amesema Kindoki.

Kindoki alianza kwa kuruhusu 'hat-trick' mchezo wake wa kwanza dhidi ya Stand United uliochezwa Uwanja wa Taifa licha ya Yanga kushinda kwa mabao 4-3.


1 COMMENTS:

  1. Kuokoa penati tu ndio kujitathimini kuwa kiwango kimepanda!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic