April 15, 2019


WACHEZAJI wa kikosi cha Simba wameomba radhi kwa mashabiki wa Simba na Taifa kwa ujumla kwa kushindwa kutimiza ndoto za kutinga hatua ya nusu fainali ila wameahidi kuendelea kupambana kurejea msimu ujao.

Simba juzi ilitolewa na TP Mazembe kwa kufungwa mabao 4-1 hatua ya robo fainali hali iliyozima ndoto zao za kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa.

Wakizungumza na Saleh Jembe kwa nyakati tofauti wachezaji hao wa Simba wamesema kuwa wanajua maumivu ya mashabiki pamoja na Taifa ila haikuwa bahati yao kusonga mbele.

Meddie Kagere ambaye ni mshambulaji mwenye mabao sita ligi ya mabingwa amesema kuwa walipambana ila walishindwa kupata matokeo.

"Mashabiki watuwie radhi haikuwa bahati yetu, tumepambana na tumeshindwa, bado tuna nafasi ya kurudi hivyo tutakuwa tumepata uzoefu na tutafanya vizuri," amesema Kagere.

Mohamed Hussein 'Tshabalala ambaye ni nahodha msaidizi amesema kuwa tayari wameonja ladha ya utamu wa mashindano ya ligi ya Afrika hivyo wanajipanga kurejea kwenye ushindani msimu ujao.

Mlinda mlango namba moja Aish Manula amesema kuwa haikuwa malengo yao kuishia hatua hiyo ila ni matokeo watapambana kurejea kwenye hatua hiyo msimu ujao.

Ili Simba waweze kurejea kwenye ligi ya mabingwa ni lazima watwae kombe la ligi kuu ambalo kwa sasa nalo ushindani umekuwa mkubwa kwani kinara ni Yanga mwenye pointi 74 huku Simba akiwa nafasi ya tatu na pointi 57.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic