UONGOZI wa Singida United umeamua kuwapa siku 10 za mapumziko wachezaji wake ili kurejea kwenye familia zao pamoja na kupata muda wa kupumzika kwa muda.
Singida United iliyo chini ya kocha Felix Minziro ilishindwa kubeba pointi tatu kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya KMC uliochezwa uwanja wa Namfua kwa kugawana pointi mojamoja.
Ofisa Habari wa Singida United, Cales Catemana amesema kuwa ligi imekuwa na ushindani hivyo wameamua kuwapa mapumziko wachezaji wapate akili mpya.
"Tunatambua kwa sasa bado mwenendo wetu haujawa mzuri ila bado tunapambana kurejea kwenye ubora, kwa sasa tumeamua kuwapa mapumziko ya siku 10 wachezaji ili wakirejea wawe na ari mpya.
"Mchezo wetu unaofuata ni dhidi ya Stand United ya Shinyanga hivyo baada ya kurejea kambini tutaanza kujipanga kwa ajili ya mchezo huo," amesema Catemana.








0 COMMENTS:
Post a Comment