April 17, 2019


NAHODHA wa timu ya Simba, John Bocco amesema kuwa kwa sasa haoni kitakachoizua Simba kutwaa ubingwa kutokana na mbinu ambazo wamezipata kwenye michezo ya kimataifa ambayo wameshiriki.

Simba walitinga kwenye hatua ya robo fainali ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuitungua mabao 2-1 AS Vita ya Congo na ndoto zao za kutinga hatua ya robo fainali zilizimwa na TP Mazembe baada ya kufungwa mabao 4-1 mchezo wa pili nchini Congo.

Bocco amesema kuwa wamejifunza mbinu nyingi kwenye michuano ya kimataifa hali itakayowafanya wacheze kimataifa kutetea kombe lao ili kurejea tena ndani kwenye michuano ya kimataifa.

"Wachezaji wote tumeona na tumegundua namna ushindani kimataifa ulivyo hivyo tunaingia kwenye ligi kuu akili zetu zikiwa michuano ya kimataifa na hatuwezi kurejea huko kama tutashindwa kubeba kombe hivyo ni lazima tushinde mechi zetu zote.

"Kombe kwa sasa bado lipo mikononi mwetu ndio maana tunaitwa mabingwa watetezi hivyo mashabiki wasikate tamaa wachezaji wao tupo tayari, na kilicho mkononi mwetu ni kombe hatuna kitu kingine tunawaomba waendelee kutupa sapoti," amesema Bocco.

Simba inaingia kwenye vita vikali vya kushindana na Yanga pamoja na Azam kuingia kwenye michuano mikubwa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa wote kuwania ubingwa wa ligi kuu.

1 COMMENTS:

  1. jamani jamani Simba na TP Mazembe wamecheza Robo Fainali mshindi ameingia nusu fainali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic