YANGA leo watashuka uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, saa nane kamili mchana kumenyana na kikosi cha Mtibwa Sugar mchezo wa ligi huku wakiwa na mtambo wa kutengenezea mabao Ibrahim Ajibu ambaye hakuwa uwanjani kwa muda wa dakika 450.
Ajibu alikosa mchezo wa Yanga dhidi ya Lipuli FC ambao ulikuwa wa ligi na Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, Alliance ule wa Shirikisho Yanga ilishinda mabao 2-1, Ndanda FC ambao Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1, African Lyon Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 na Kagera Sugar ambao Yanga ilishinda mabao 3-2 kutokana na kutokuwa fiti kiafya.
Ajibu amehusika katika mabao 15 ndani ya Yanga na pia amefunga mabao 6 huku kati ya hayo 15 manne amempatia kinara wa kufumania nyavu mwenye mabao 15 ndani ya Yanga, Heritier Makambo.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kuwa kwenye mchezo wake wa leo atakuwa na maingizo mapya mawili na atawakosa pia wachezaji wake wawili hivyo hakuna kilichoharibika.
"Nitawakosa wachezaji wawili leo ambao ni Kelvin Yondan mwenye kadi nyekundu na Feisal Salum mwenye kadi tatu za njano ila hakuna kilichoharibika tayari beki Abdallah Shaibu 'Ninja' amerejea na mtaalamu wa kutoa pasi za mabao kwa Makambo, Ajibu yupo fiti.







0 COMMENTS:
Post a Comment