JESHI la polisi limefanikiwa kuwatia nguvuni majambazi watatu kati ya sita wenye silaha waliovamia duka la Almore Flight Services Ltd, usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita kwa lengo la kupora mali eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi pamoja na wenzao waliokimbia baada ya mapambano makali na polisi waliofika hapo, wanaendelea kusakwa na watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Aidha, Mambosasa ametoa onyo kwa wale wote wanaokusudia kuvuruga biashara katika eneo la Kariakoo ambalo ni kitovu cha biashara nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment