April 20, 2019


Kocha wa timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys Oscar Mirambo, amesema watapambana leo mpaka dakika ya mwisho kufuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Afrika ngazi ya vijana chini ya miaka 17 yanayofanyika hapa nchini katika jiji la Dar es salaam.

Mirambo amesisitiza kuwa bado hawajakata tamaa licha ya kuwa na nafasi finyu ya kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo..

Kwa upande wake kocha wa Angola amesema wapo tayari kwa pambano hilo akiwa na matumaini ya kupata matokeo chanya kutokana na ubora wa timu yake.

Matumaini ya Serengetii Boys kwenda Brazil yalizimwa na Uganda baada ya kupoteza kwa mabao 3-0 na ukiwa ni mchezo wa pili baada ya ule wa kwanza kufungwa na Nigeria mabao  5-4.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic