May 8, 2019



BAADA ya kikosi cha Lipuli kushinda mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga kwa ushindi wa mabao 2-0, kocha Seleman Matola amesema kuwa hajafurahia ushindi huo.

Ushindi huo unakuwa ni wa pili mfululizo kwa Lipuli katika mechi za hivi karibuni uwanja wa Samora, kwani kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara alishinda bao 1-0 na juzi alishinda mabao 2-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema anawapongeza wachezaji wake kwa kufuata maelekezo ila walikuwa na nafasi ya kufunga mabao zaidi ya matano kwenye mchezo huo.

"Mchezo ulikuwa mgumu na wenye ushindani ila tulikuwa na nafasi ya kufunga mabao matano, haikuwa bahati yetu kushinda mabao mengi ila nashukuru tumepata mawili sio mbaya kwetu.

"Yanga ni timu ngumu ila ukiwabana unapata matokeo na ndivyo nilivyofanya baada ya kauza kuwafunga mapema walijivuruga wenyewe kisha tukapeta," amesema Matola.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa kikosi cha Lipuli kutinga hatua ya fainali ya kombe la Shirikisho ambapo bingwa wa michuano hii anaiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.

1 COMMENTS:

  1. Habari za Kazi
    Mimi ni mtanzania ninayeishi nje ya nchi....nimekuwa nikiifuatilia sana Yanga...na ningependa kutoa pongezi kwa kuweza kupata uongozi mpya....hapa chini nimefanya tathmini fupi na kubainisha nini kifanyike ili msimu ujao muweze kuchukua ubingwa

    1. Uongozi utathmini maendeleo na kwanini timu haijafanikiwa....ingawa ni kweli kuwa huyo kocha amewasaidia lakini lazima kuwepo na "check and balance" asiaachiwe saana na asiingiliwe saana pia, kila mpenzi wa soka anakiri kuwa amejitahidi kuifikisha timu hapo ilipo, lakini ni lazima kubadilishwa na kuliimarisha benchi zima la ufundi kwa mustakabali wa maendeleo ya klabu kufikia malengo yake...msiridhike kwakuwa mnaongoza au mliongoza ligi kwa muda mrefu na mlifikia nusu fainali ya FA, bado wanayanga wana machungu na maumivu ya kushindwa kuchukua kombe la FA. 
    2. Ukweli ni kwamba timu ina mapungufu mengi sana....caliber ya wachezaji wa Yanga wengine hawakufaa kuwemo kwenye hii timu wengi wao viwango ni vya chini mno, na umri umesogea mno. Pia mwalimu wa viungo, kocha wa makipa, madaktari, mameneja na wachua misuli....bado ni wa level ya chini hawana tofauti na wa timu za Ndanda, Alliance nk....usajili na viwango vya professional players ni duni....ndio unaweza ukadai kuwa tatizo ni pesa lakini hata hivyo baadhi yao hata scouting was very poor, na hawakuwa fiti, kuporomoka kwa uchezaji wao na umri umesogea mno, wachezaji wengi wazawa pia kuna kushuka kwa viwango kama ilivyo kwa wageni......timu kama Lipuli siyo ya kuitoa Yanga....yaliyopita si ndwele sasa mugange yajayo....
    3. USAJILI WA KIWANGO CHA JUU NA KULIIMARISHA BENCHI LA UFUNDI....Challenge ni kushawishi wachezaji waliopo ambao wameibeba timu kubaki kikosini....kwa kusaini mikataba mipya!....Kuhusu Uwezo wa Mwalimu Noeli Mwandila....sidhani kama unaridhisha....kila ambapo Mwalimu Zahera akiondoka kwenda kwenye timu ya Taifa Kongo....akirudi viwango vya wachezaji vinakuwa chini mno....physical fitness is very low!...lazima ili liangaliwe....madaktari pia wachezaji walio majeruhi Yanga huchukua muda mrefu kupona....nadhani kuna haja ya kuipa uwezo na vifaa vya kisasa idara ya utabibu....yako madhaifu mengi mfano mengine kama kutokuwepo kwa ubora wa kambi na viwanja vya mazoezi, na kadhalika lakini haya ndio ya msingi....
    4. Sasa mengine yalichangiwa na uongozi dhaifu na uchumi kudorora sasa hivi au msimu ujao hilo lisiwe tena kisingizio!
    Ahsante,

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic