BAADA ya Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kujirekodi video na kuweka ahadi kwamba endapo timu ya Liverpool ya England ikiifunga timu ya Barcelona ya Hispania kwenye Ligi ya Mabingwa atahamia Yanga uongozi wa Yanga umemkataa.
Manara alisema kuwa atahamia Yanga rasmi na kuisaidia kuchangisha fedha kwa moyo mmoja na kuvaa jezi yao na usiku wa leo Liverpool waliitoa Barcelona uwanja wa Anfield kwa kuifunga mabao 4-0 hali iliyofanya waitoe kwa idadi ya mabao 4-3.
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa hana mpango wa kumpokea mwanachama huyo mpya kwa kuwa amezoea kubebwa na asitarajie kuwa ndani ya Yanga.
"Duniani kote hakuna mtu anayekubali kubebwa kwenye mpira, inafaa kusamehewa naomba mumsamehe kwa kuwa hawezi kuwa ndani ya Yanga, amezoea kubebwa ataifanya na timu yangu ianze kupenda kubebwa," amesema.
Zahera usijitoe kimasomaso tunakutaka uongelee waziwazi kipigo cha mbwa Koko ulichokipata kutoka Lipuli baada ya kuahidi kuifunga Lipuli dakika 15 za mwanzo kwani unaropokwa bila ya kujijuwa
ReplyDeleteManara is great entertainment
ReplyDeleteHahaha ndio kweli kasadiki kuwa Manara atajiunga na yanga. Huyu MTU WA Mikasa Mingi, yeye ndie muamuzi WA kila kitu WA yanga bila ya kushauri au hata kuuliza
ReplyDeleteHabari za Kazi
ReplyDeleteMimi ni mtanzania ninayeishi nje ya nchi....nimekuwa nikiifuatilia sana Yanga...na ningependa kutoa pongezi kwa kuweza kupata uongozi mpya....hapa chini nimefanya tathmini fupi na kubainisha nini kifanyike ili msimu ujao muweze kuchukua ubingwa
1. Uongozi utathmini maendeleo na kwanini timu haijafanikiwa....ingawa ni kweli kuwa huyo kocha amewasaidia lakini lazima kuwepo na "check and balance" asiaachiwe saana na asiingiliwe saana pia, kila mpenzi wa soka anakiri kuwa amejitahidi kuifikisha timu hapo ilipo, lakini ni lazima kubadilishwa na kuliimarisha benchi zima la ufundi kwa mustakabali wa maendeleo ya klabu kufikia malengo yake...msiridhike kwakuwa mnaongoza au mliongoza ligi kwa muda mrefu na mlifikia nusu fainali ya FA, bado wanayanga wana machungu na maumivu ya kushindwa kuchukua kombe la FA.
2. Ukweli ni kwamba timu ina mapungufu mengi sana....caliber ya wachezaji wa Yanga wengine hawakufaa kuwemo kwenye hii timu wengi wao viwango ni vya chini mno, na umri umesogea mno. Pia mwalimu wa viungo, kocha wa makipa, madaktari, mameneja na wachua misuli....bado ni wa level ya chini hawana tofauti na wa timu za Ndanda, Alliance nk....usajili na viwango vya professional players ni duni....ndio unaweza ukadai kuwa tatizo ni pesa lakini hata hivyo baadhi yao hata scouting was very poor, na hawakuwa fiti, kuporomoka kwa uchezaji wao na umri umesogea mno, wachezaji wengi wazawa pia kuna kushuka kwa viwango kama ilivyo kwa wageni......timu kama Lipuli siyo ya kuitoa Yanga....yaliyopita si ndwele sasa mugange yajayo....
3. USAJILI WA KIWANGO CHA JUU NA KULIIMARISHA BENCHI LA UFUNDI....Challenge ni kushawishi wachezaji waliopo ambao wameibeba timu kubaki kikosini....kwa kusaini mikataba mipya!....Kuhusu Uwezo wa Mwalimu Noeli Mwandila....sidhani kama unaridhisha....kila ambapo Mwalimu Zahera akiondoka kwenda kwenye timu ya Taifa Kongo....akirudi viwango vya wachezaji vinakuwa chini mno....physical fitness is very low!...lazima ili liangaliwe....madaktari pia wachezaji walio majeruhi Yanga huchukua muda mrefu kupona....nadhani kuna haja ya kuipa uwezo na vifaa vya kisasa idara ya utabibu....yako madhaifu mengi mfano mengine kama kutokuwepo kwa ubora wa kambi na viwanja vya mazoezi, na kadhalika lakini haya ndio ya msingi....
4. Sasa mengine yalichangiwa na uongozi dhaifu na uchumi kudorora sasa hivi au msimu ujao hilo lisiwe tena kisingizio!
Ahsante,