May 27, 2019


Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Crescentius Magori amewashangaa watani zake wa jadi Yanga kuhusu ucnagishaji wa fedha wanaoufanya hivi sasa.

Magori amekuja na kauli kufuatia harambee maalum ambayo imekuwa ikifanywa na watani zao hao wa jadi ili kuisaidia klabu isonge mbele kimaendeleo kutokana na hali wnaayopitia.

CEO huyo wa Simba amesema Yanga wanakuwa kama hawana udhamini huku akiitaja kampuni ya bahati nasibu ya SportPesa kuwa mdhamini wa timu za Simba na Yanga.

Amesema anashangazwa kwa namna Yanga wanavyohangaika kuchangisha fedha ilihali SportPesa wanatoa fedha ambayo inaenda pia Yanga.

Aidha amedokezea kuwa wakati Yanga inafadhiliwa na Yusuf Manji wao walikuwa wanategemea zaidi kikosi cha vijana ikiwemo wachezaji kama William Lucian, Jonas Mkude, Said Ndemla na Ibrahim Ajibu ambao waliwapandisha mpaka kikosi cha kwanza.

Amemaliza kwa kusema ni vema Yanga wakaangalia namna nyingini ikiwemo fedha ambazo wanazipata kutoka kwa wadhamini wao ili kuindesha klabu zaidi ya kutegemea michango.


10 COMMENTS:

  1. Nasaha muwafaka lakini utaonekana adui. Ikiwa Yanga ndio mojakwamoja inategemea pesa ya bakuli ifahamu kuwa misaada ina ukomo wake na nirahisi Sana kupata wachezaji WA kiwango cha juu lakini si rahisi kuwatimizia haja zao Kwa pesa ya bakuli na hapo tena ndipo yanapotokeza matatizo ya migomo isiyokwisha na kufukuzwa wanaodai Chao. Nguo ya kuomba haisitiri makalio.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu zangu mfanye tafakari moja kubwa sana, yule muhindi MO bado hajaweka ile hela aliyoahidi. Anatoa pesa zake mfukoni tu. Inatakiwa muanze kutembea kifua mbele akiweka hiyo pesa kwa maana italeta manufaa hata asipokuwepo. Yule ni binadamu jamani haaya!! Kabla hujatoa povu fanya tafakari kwa kina. Yanga tulilemaa na pesa za mfukoni za Yusuf alafu wehat next. Ni jambo la kujifunza sio kudhihaki tuu au kuwashambulia Yanga. Hii nchi haieleweki, sijawahi kuziamini tawala za kiafrika kamwe. Haya jamani

      Delete
  2. wao walivyokuwa wanachangishana kundi la Freinds Of Simba akumbuki sio wakati wa usajili na zile walizokuwa wanachangishana na kuikopesha simba, mambo ya Yanga waachie wenyewe au mnataka muwaburuze kama msimu unaishia kesho.

    ReplyDelete
  3. Mtaburuzwa kuliko msimu uliopita .Kwa hiyo kuchangishana kwa Friends of Simba wakati huo ndio role model ya Yanga kwa sasa?Ulikuwa mfumo mbovu usio sustanaible na unakaribisha migogoro.Uwekezaji ndio solution sio michango isio na guarantee.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Iko hivi, wana Yanga walikuwa wanasubiri uchaguzi upite, ligi imeisha, then kinachofuata ni majadiliano ya wanachama mfumo upi unafaa. Subirini mmeanza nasi tunamaliza.

      Delete
  4. Magori hana akili au anaongea kishabiki, simba walikuwa wanachangishana katika usajili na kuna wakati walikuwa wanashindwa hata kulipa mishahara. Ni ujinga kusema kuwa walikuwa wanategemea kikosi cha vijana, je hicho kikosi kiliwafikisha wapi, si ndo kikosi kilichowafanya wakakaa miaka minne bila ubingwa na wala kishiriki mashindano ya kimataifa? Yeye azungumzie mikakati yake, Sportspesa wanatoa sh ngapi? mbona wao hawakutumia hiyo hela kusajili na matokeo yake muda wote wanalia MO utafikiri ng'ombe?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwahiyo una hasira kuambiwa wewe si masikini?

      Delete
    2. Kwani nyie matajiri??

      Delete
  5. Umekiri mwenyewe kuwa Simba walipokuwa wanachangishana walikaa miaka 4 bila ubingwa,hivyo Yanga nao wajiandae kukaa miaka hiyo au zaidi kwa mtindo huo wa kuchangishana, kwani mtindo huu hautaisaidia timu

    ReplyDelete
  6. Haijurudii tena sheikh, mmetubahatisha misimu hii miwili inatosha. Ngojeni tu. Tatizo mkikaa wenyewe mnajipigia hadithi na kufarijiana!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic