May 13, 2019


Kama wewe ni mchezaji mzawa na unataka kusaini Yanga, usiote ndoto za milioni 50 wala milioni 100 utakuwa unajisumbua. Dau la safari hii halizidi Sh milioni 30 na ndiyo msimamo wa Kocha Mwinyi Zahera na uongozi mpya.

Imebainika kwamba, wachezaji 13 pekee wa zamani ndiyo wako salama kwenye usajili mpya, lakini kuna 10 wanaokwenda na maji ambao listi yao inashtua kidogo na kutia huruma.

Uongozi huo mpya chini ya Mwenyekiti Mshindo Msolla, ulipanga kukutana na Zahera mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United, jana Ijumaa kwenye Uwanja wa Karume huko Mara.

Habari zinasema kwamba kocha ameshadokeza kwamba wachezaji ambao hawakucheza nusu ya mechi msimu huu unaoelekea ukingoni wanakwenda na maji.

Takwimu za mechi za Yanga zinaonyesha kwamba wachezaji hao 10 walioko kwenye hatari ni Anthony Matheo, Baruhani Akilimali, Juma Mahadhi, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haji Mwinyi, Said Makapu, Deus Kaseke na Ibrahim Hamid kipa aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili msimu huu wakati Beno Kakolanya yeye ameshaachana na timu hiyo.

Mbali na hao, wapo mastaa wengine ambao watatolewa kwa kigezo cha ufanisi mdogo wakiongozwa na kipa Klaus Kindoki.

“Uongozi mpya ulikutana na kocha na kufanya naye kikao kifupi mara baada ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA na Lipuli FC kumalizika na kikubwa walitaka kufahamu sababu ya kipigo hicho na kuwaambia kuwa hana kikosi imara cha ushindani.

“Na kuwagusia mipango yake ya kuisuka Yanga imara itakayokuwa tishio ikiwemo kuwatema wachezaji ambao hawakucheza nusu ya mechi katika msimu huu huku akiahidi kubaki na wale waliocheza michezo mingi na kuwasajili wapya watakaoleta ushindani wa namba katika kikosi chake.

“Hivyo, mara baada ya mchezo dhidi ya Biashara haraka viongozi watakutana na kocha kuwakabidhi bajeti yake ya usajili ambayo kwa kila mchezaji mzawa atasaini kwa dau la chini ya Shilingi mil 30 huku wakimataifa wakiandaliwa dau lao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa mwenyekiti Msolla kuzungumzia hilo simu yake ya mkononi ilikuwa bize lakini makamu wake Fredrick Mwakalebela alisema; “Tumepanga kukutana na kocha kujadiliana mipango ya usajili na vitu vingine baada ya mchezo wetu na Biashara, hayo mengine kama yapo yatajitokeza.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Huyu Kocha ndio maana anatakiwa asimamiwe na asiwafanye Yanga wote ni wajinga haiwezekani atamke kuwa eti atasajili wachezaji 8 tu....hata asiye na akili na soka anaelewa kuwa Yanga imekuwa dhaifu mno na zaidi ya 3/4 ya wachezaji waliopo kikosini hawafai hata kuendelea kubaki Yanga....sasa atakujaje na kusema atasajili wachezaji 8 tu? Ndio maana wanayanga wanahamasishwa kuchangia na kukusanya fedha ili waunde timu imara na kusajili wachezaji bora wa kutosha waondokane na hali iliyopo...tatizo halitakuwa pesa tena kwani watakuwa na fedha ya kutosha kusajili na kulipa mishahara....asiwafanye wanayanga warudi kule walipotoka kwa kuwa na kikosi dhaifu chenye wachezaji wa nje na ndani ya nchi ambao wengi wao ni magarasa wa kiwango cha chini ambao hata wakicheza na Lipuli, Ndanda, Singida United wanafikiria "kupaki basi". Yanga wanataka wachezaji wa kiwango cha juu mno wakushindana na kutoa upinzani wa hali ya buy kwa timu kama Simba, TP Mazembe, Al Ahly nk...hata kama hawata shiriki mashindano ya CAF lakini wataisaidia kuchukua ubingwa wa ligi hayo ndio matamanio na mahitaji yao wapenzi na wakereketwa wa Yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic