May 27, 2019


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa umekaa kikao na wachezaji wote wa Mtibwa kuelekea kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Simba utakaochezwa uwanja wa Jamhuri na kukubaliana kwamba ni lazima Simba apigwe.

Mtibwa Sugar, kwenye michezo yake mitatu mfululizo hajawa na matokeo chanya kwani alianza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Coastal Union, kabla ya kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Simba na mchezo wa mwisho alifungwa mabao 2-0 na Azam FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa matokeo mabaya waliyoyapata yatafutwa na Simba ambao watawafuata Jamhuri.

"Tumepigwa sana mechi hizi za mwisho, tumepoteza furaha kiasi cha kutosha sasa ni zamu yetu kurejesha tabasamu, hivyo Simba atatusamehe tu lazima apigwe Jamhuri.

"Ni mchezo wetu wa mwisho kwa ajili ya kujipanga kwa msimu ujao, tuna imani tukishinda tutajiweka nafasi nzuri ya kumaliza tukiwa ndani ya tano bora sasa ni lazima tulipe kisasi kwa Simba," amesema Kifaru.

Simba ambao ni mabingwa mchezo wao wa kesho wanatarajiwa kukabidhiwa kombe baada ya sherehe hizo zilizopangwa kufanyika Dar kughairishwa kutokana na mgeni rasmi Kangi Lugola kupata udhuru.

2 COMMENTS:

  1. Yetu macho na masikio hamchelewi kusema Simba imebebwa.

    ReplyDelete
  2. Siyo tu kubebwa ila kununua mechi kabisa.Kumbukeni mlivyojinasibu wakati wa mechi ya kwanza ambayo yalitokea mkabaki kinywa wazi na kusema marefa hawafuati sheria 17 za mchezo.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic