May 27, 2019

KIUNGO wa Yanga, Papy Tshishimbi ambaye ameongeza mkataba wa miaka miwili ndani ya Yanga amesema kuwa kinachomfurahisha ndani ya kikosi hicho ni ushirikiano uliopo.

Tshishimbi kwa sasa amekuwa ni mchezaji wa kwanza kuwa na uhakika wa kubaki kwenye kikosi hicho msimu ujao amesema ana furaha kuwa ndani ya Yanga kutokana na aina mashabiki waliopo.

"Ninafurahi kuwa ndani ya Yanga kutokana na aina ya mashabiki ambao wapo wanajali na wapo bega kwa bega nasi muda wote ni furaha kwangu na timu.

"Pia jambo jingine ni kutokana na ushirikiano uliopo ndani ya kikosi kwani kila mmoja anatoa ushirikiano ndio maana nimekuwa nikifanya vizuri bila ya kujali ninacheza na nani uwanjani," amesema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic