May 8, 2019


Beki wa kulia wa kikosi cha Simba SC , Zana Coulibally kesho atakosa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union kufuatia kuwa na kadi tatu za njano.

Zana ataikosa mechi hiyo kutokana na kadi hizo ambapo moja kati ya hizo aliipata kwenye mchezo wa Kombe la FA Simba ilipocheza na timu ya Mashujaa FC ya mkoani Kigoma.

Kadi nyingine mbili amezipata kwenye mechi za ligi kuu Bara ukiwemo mchezo wa mwisho dhidi ya Tanzania Prison.

Kwa mujibu wa kanuni, ikimbukwe kuwa ukipata kadi kwenye michezo ya FA itahesabika mpaka kwenye michuano ya ligi kuu.

Hivyo hivyo pia, ukipata kadi kwenye ligi kuu basi adhabu itatumika mpaka FA na kufutika kwa kadi ni mpaka pale utakapotumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja hata kama ni mwakani .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic