MANARA AJA NA JIPYA SIMBA
Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameirejesha tena kauli mbiu ya DO OR DIE kwenye mechi tano za ligi kuu Tanzania Bara ambazo zitafanyika katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.
Manara amesema hawana budi kuzifanya mechi zao tano dhidi ya (Coastal May 08, Kagera May 10, Azam May 13, Mtibwa May 16 na Ndanda May 19) kuwa vita ili washinde zote na watangaze ubingwa mapema.
Aidha, Manara ameongeza kuwa watapeleka maombi kwenye shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuomba ubingwa huo wakabidhiwe May 23 kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Sevilla ya Hispania.
Ikumbukwe Simba waliitumia kauli hiyo mara ya mwisho katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambayo ilimalizika kwa matokeo ya 0-0.
liva kashamtoa fcb tunakungoja jangwan
ReplyDeleteehee tunakusubiri na chupa za mkojo tukukaribishe jangwani.
ReplyDeleteAlikuwa anatania. Washamba msilishikie bango.
ReplyDeleteKumbe mnataka eeeh,nyoo hammpati ng'oooh atawachangia tu basi
ReplyDeleteManara aende Yanga!!!! Akafanye nini huko?
ReplyDelete