May 16, 2019

JOHN Bocco nahodha wa Simba leo amefunga bao lake la 15 kwenye ligi kuu Bara kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru akimalizia pasi ya Meddie Kagere dakika ya 33.

Bao lake la leo linakamilisha jumla ya mabao 113 kwenye soka hali inayomfanya azidi kuwa mshambuliaji mwenye urafiki na nyavu kwa bongo.

Mabao mengine ya Simba leo yamefungwa na mwamba wa Lusaka, Clatous Chama dakika ya 48 baada ya mabeki wa Mtibwa Sugar kujichanganya na bao la tatu limepachikwa na  Emmanuel Okwi dakika ya 56.

Ushindi huo unairejesha Simba kileleni kwa kuishuhsa Yanga ambayo ilikuwa kileleni baada ya kufikisha jumla ya pointi 83 huku Simba ikifikisha jumla ya pointi 85.

Simba wanafikisha jumla ya pointi 84 wakiwa wamefunga jumla ya mabao 72 huku kinara wa upachikaji wa mabao akiwa ni Meddie Kagere mwenye mabao 20 kwa sasa ligi kuu Bara.

Simba imebakiwa na michezo minne ili kukamilisha mzunguko wa pili msimu huu ambapo mpaka sasa wamebakiza pointi tano ili kuweza kutetea ubingwa wao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic