May 16, 2019



WABABE wa Simba msimu huu, Kagera Sugar ambao waliifunga Simba nje ndani na kuwa timu ya kwanza kubeba pointi sita leo wamepoteza mchezo wao mbele ya Stand United kwa kufungwa mabao 3-1 mchezo uliochezwa uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Stand United walianza kucheka na nyavu mapema dakika ya 3 kipindi cha kwanza kupitia kwa Charles Chinonso kabla ya mshambuliaji machachari wa Kagera Sugar, Kassim Khamis kusawazisha bao hilo dakika ya 45.

Kipindi cha pili Jacob Masawe dakika ya 48 alipachika bao la pili kabla ya  bao la tatu la ushindi kupachikwa dakika ya 90 na Datius Peter lililoipa pointi tatu timu yake ya Stand United.

3 COMMENTS:

  1. kumbe hovyooo...ikifika Simba unaweka nguvu ambazo ungetumia muda lote ungemaliza ligi wa pili..Ni kama mbao vile

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeonaa enhee...ndio udhaifu wa timu zetu aliosema kocha wa Simba.Unapania na kukaza msimu wote wa ligi kwa timu ya Simba tu na kujisifu lkn ni mlendaa tu kwa timu nyingine.Hovyooo kabisa

      Delete
  2. Pumbafu hawa.. Yn hzi timu ndio maana zinakaribia kishuka daraja.. Unajiuliza hivi simba na stand ipo ni bora? Kwli mpira una matokeo katili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic