May 8, 2019



Katika kuhakikisha inazidi kuwafurahisha wateja wake, Kampuni ya Michezo ya Kubashiri Tanzania, SportPesa Tanzania leo imezindua promosheni mpya inayofahamika kama ‘USIBAHATISHE CHEZA NA SPORTPESA’.


Promosheni hiyo itakuwa ya kushindania gari ndogo tatu (3) aina ya IST, Simu janja za kisasa Smartphone 200, tiketi 45 za mechi ya Simba dhidi ya Sevilla FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) na tiketi 10 za mchezo wa Kariobangi Sharks na Everton ya England utakaochezwa nchini Kenya.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema wamezindua promosheni hiyo ambayo imeanza toka Mei Mosi na itakuwa kwa wiki 15, kwa malengo ya kampuni kuzidi kuwa karibu na wateja wake.


“Tumezindua promosheni mpya inayokwenda kwa jina la ‘Usibahatishe Cheza na SportPesa’, ambayo tutatoa magari matatu (3) ya kisasa kabisa aina ya IST.


“Lakini tutatoa zawadi ya simu za kisasa pia Smartphone 200 ambazo zitaenda kwa wateja wetu watakaoshinda katika droo tutakazochezesha,” anasema na Tarimba na kuongeza.


“Pia, tutatoa tiketi 45 za mechi ya Simba ambayo itacheza na mabingwa wa Hispania (La Liga), timu ya Sevilla ambao watacheza tarehe 23 mwezi huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Lakini tutatoa tiketi zingine 10 za kwenda kuangalia mechi ya timu ya Kariobangi Sharks watakaocheza na Everton ya England watakaocheza nao kule Kenya.


“Promosheni hii itachezeshwa kwa droo 15 kwa wiki 15 kwa kuwapata washindi. Hivyo kila siku ukibeti unashinda zawadi, sasa huu ni wakati wa Watanzania kuchangamia fursa hiyo,” anasema.


Tarimba, anasema kuwa leo wameanza kwa kutoa simu za Smartphone sita (6) na tiketi za mechi ya Simba dhidi ya Sevilla 13, baada ya kuibuka washindi wa droo ya kwanza.


“Tunajisikia faraja kurudisha fadhila kwa Watanzania, hasa wateja wetu, sasa huu ni wakati wao kucheza zaidi na SportPesa ili kujishindia zawadi zetu hizi mpya za gari, simu na tiketi za mechi hii kubwa ya Simba na Sevilla,” anasema.


 Sevilla inatarajia kuwasili nchini Mei 21, kisha kucheza na Simba Mei 23 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kufuatia mwaliko wa kampuni ya michezo ya kubahatisha nchini, SportPesa Tanzania.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic