May 8, 2019


Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewasilisha malalamiko mbalimbali ya kinidhamu dhidi ya viongozi, makocha na wachezaji kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 

Walalamikiwa ni kutoka katika klabu za Ligi Kuu ya Tanzania (TPL), na Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Makocha waliolalamikiwa ni Athuman Bilal wa Stand United, Mwinyi Zahera (Yanga), Nassoro Mrisho (Geita Gold FC), na Ramadhani Nsanzurwimo (Mbeya City).

Viongozi ni Herry Chibakasa wa Friends Rangers FC, Mohamed Hussein (Kagera Sugar FC),Walter Harrison (KMC) na Hussein Salehe wa Geita Gold FC wakati mchezaji aliyelalamikiwa ni Deus Tulusubya wa Pamba SC.

Kamati ya Nidhamu ya TFF itakutana Mei 12,2019

5 COMMENTS:

  1. Hivi Zahera alikumbuka kupiga picha msimamo wa ligi TPL kwa maana hata waona Yanga pale kileleni!TENA!

    ReplyDelete
  2. Ukimuangalia Othmani khazi na kipindi chake cha kipenga cha mwisho basi utajua kuwa Yanga ndio timu inayobebwa na waamuzi na Simba anaangushiwa tuhuma feki zisizostahili kabisa. Lakini hii ndio bongo. Yanga hawana njia nyengine ya kujitetea baada ya kupoteza muelekeo kwenye ligi isipokuwa kuendesha kampeni ya kusema Simba anabebwa wakati picha zote za marejeo kwenye t.v. kutoka kwa waamuzi wataalam zinaonesha hakuna mahali ambapo Simba kabebwa.

    ReplyDelete
  3. Yanga msimu Ni mbovu Sana na happy alipofikia Ni Kama zali tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic