May 8, 2019

2 COMMENTS:

  1. Barcelona,Mesi,Barcelona,
    Barcelona. Nimeitaja mara kadhaa hapo juu Barcelona kwenye ujumbe wangu huu mfupi pengine hakuna hata atakaejishughulisha kuusoma ila anaekwenda tofauti na aliekaa na kwa mantiki hii mawazo ya hovyo yaliyowasilishwa huwa na maana kuliko mawazo sukari yaliyoshindwa kuwasilishwa.
    Mechi hii ya Liverpool na Barcelona ina mafundisho mengi sana kwa tasnia ya mpira Tanzania.
    (1)Mpira kocha bana.
    (2)Midfield ama wachezaji wa viungo hasa wa kati, Fabinho wa Liverpool jinsi alivyokuwa akicheza kama vile hataki kuishi tena katika Dunia hii seuze kujali kupata yellow kadi au red card.kwa kweli ameonyesha vipi kiungo mkabaji anatakiwa kufanya kazi yake .
    (3) wachezaji wa akiba. Wachezaji wa akiba wa Liverpool ambao sio chaguo la kwanza la kocha wameonesha jinsi gani mchezaji anatakiwa kufanya ili arejeshe imani ya kocha na kumuamini. Sio hawa wachezaji wetu wa kitanzania anakaa benchi siku kocha anaamua kumpa namba basi kocha anatamani kumtoa hapohapo.
    (4)kujiamini, Wachezaji wana takiwa kujiamini wao wenyewe binafsi kwanza kuwa wanauwezo wa kufanya makubwa na kutekeleza kwa vitendo. Kocha wa Liverpool amekiri kuwa hakuwa akidhani kama kweli vijana wake wanaweza kupindua meza mbele ya Baerclrona ila Kapteni wa Liverpool Jordani Henderson amesema wachezaji wa Liverpool wao walikuwa wanajiamini kabisa kuiondosha nje ya mashindano Barcelona pale Anfield.
    (5)Imani ya mashabiki juu ya timu yao kama ingekuwa hapa kwetu baada ya timu kukubali tatu mtungi na timu kama Barcelona pengine hata mashabiki wasingekwenda uwanjani. Lakini kubwa kuliko yote kwenye mpira chochote kinaweza kutokea na tukirudi nyuma kunako klabu bingwa Africa utaona wachambuzi wengi wa soka Tanzania hawakuwa wakiitendea haki Simba kwani uchambuzi wao mwingi ulijikita katika kuwapamba wapinzani wa Simba na kwa kiasi fulani naweza kusena uchambuzi huo ulichangia sana kuiondoshea Simba na wachezaji wake hali ya kujiamini kwa timu pinzani.Inajulikana kabisa hulka ya Mtanzaia kusifia vya kigeni hata kama vya hovyo ila kunako vita tahadhari ni lazima ila kamwe huwezi kulijengea mazingira ya uoga jeshi lako hata kama mpinzani wenu yupo vizuri kiasi gani.Ingefurahisha kwa wachambuzi wetu wa soka kuona wanakwenda deep zaidi kutoa chambuzi zinazoelekeza nini cha kufanya kwa timu zetu zinapokutana na timu ambazo tunadhani zipo juu kisoka kuliko timu zetu na sio kukomalia kuzisifia tu hizo timu za kigeni. Mfano Ahly kaenda Africa kusini kapigwa kama mtoto mdogo lakini kwa kwetu hapa ukisikiliza jinsi wachambuzi wetu wanavyoisifia Ahly kama vile imetoka mbinguni.Na mwisho wa siku licha ya nchi yetu kuwa na ligi ya kawaida lakini ushiriki wa Simba klabu bingwa Africa imeonesha haikuwa na tofauti kubwa kiviwango na timu nyingi bora barani Africa pengine tungewaamini Simba zaidi wangefika mabali zaidi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na waandishi wetu walivyokuwa hawajielewi na kuandika Simba kunyang'anywa pointi kwa kmadai ya kupulizia madawa vyumba vya wapinzani.Mie nawashangaa viongozi wa Simba,TFF kwa nini hawakufuatilia haya madai machafu kwani inachafua taswira ya soka la Tanzania.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic