May 26, 2019

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hesabu zao kubwa ni kuona wanamaliza ligi kwa heshima hivyo wemejipanga kubeba pointi tatu mbele ya Azam FC.

Yanga itamenyana na Azam FC Mei 28 uwanja wa Uhuru ikiwa ni mchezo wa mwisho msimu huu wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa kwanza kwa bao 1-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredric Mwakalebela amesema kuwa wanaiheshimu timu ya Azam FC kutokana na ubora wao ila hakuna kitakachowazuia washindwe kushinda.

"Ligi ndo inafika ukingoni na bingwa tayari ameshapatikana kwa kuwa kwenye mashindano lazima mshindi apatikane, sasa kuelekea mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Azam FC, tupo vizuri tumejipanga kupata matokeo chanya.

"Kwa sasa hakuna cha kupoteza zaidi ya heshima tu, kama ambavyo tulianza kwenye mchezo wa awali ni lazima tumalize mchezo wetu wa mwisho kwa ushindi," amesema.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic