MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, iliyo chini ya Kocha Mkuu, Emmanuel Amunike, Kassim Hamis amepata madili makubwa kwa timu za Simba, Yanga na Azam FC ambao wanawania saini yake.
Kassim mshambuliaji wa Kagera Sugar ametimiza majukumu vyema kwa timu yake na kuitoa nafasi ya 17 mpaka nafasi ya 10 kwa sasa wakiwa na pointi 43, na yeye akifunga jumla ya mabao sita.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kassim ambaye ametingisha nyavu za vigogo wote wa ligi walio nafasi ya kwanza na ya pili, Yanga na Simba amesema kuwa amekuwa akitafutwa na viongozi wengi ili asaini kwenye timu zao.
"Nina furaha ndani ya Kagera Sugar na pia baada ya kuitwa timu ya Taifa, viongozi wa timu kubwa wamekuwa wakinifuata ili niweze kujiunga na timu zao ila kwa sasa bado nitabaki Kagera Sugar.
Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kikubwa anachowaambia wachezaji wake ni kuongeza juhudi masuala ya kujiunga na timu nyingine itakuwa baadaye.
Huyu kocha anatakiwa asimamiwe asiachiwe yeye...kusajili wachezaji kwani asije akaleta magharasa lazima alete wachezaji wa hali ya juu...wachezaji wa ndani hao pia wawe wa hali ya juu pia!
ReplyDelete