Kassim Khamis, mshambuliaji wa Kagera Sugar saini yake inawindwa na uongozi wa Yanga, Azam FC na Simba kutokana na uwezo wake mkubwa akiwa ndani ya uwanja hasa kwa kufanikiwa kumiliki mpira na kuzuia asipokonywe mguuni.
Kassim alimvutia kocha mkuu wa Timu ya Tanzania, 'Taifa Stars' Emanuel Amunike kabla ya kumtema dakika za usiku wakati kikosi kinakwea pipa kwenda Misri.
Akizungumza na Saleh Jembe, Khamis amesema kuwa amekuwa akizungumza na viongozi wa timu tofauti wakihitaji kuipata saini yake.
"Ni timu nyingi nimekuwa nikiwasiliana nazo kwa ajili ya kujadili kuhusu mkataba wangu, wakati ukifika nitataja timu ambayo nitakwenda msimu ujao na itakwa ni ile yenye manufaa kwangu.
"Najua kwamba ni lazima niwe ndani ya uwanja msimu ujao ila kusaini bila kujua hatma yangu ndani ya kikosi itakuwa ni mbaya hivyo acha nitulie kwa sasa," amesema.
Kassim jana alikuwa miongoni mwa kikosi kilichocheza dhidi ya Pamba FC na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 hivyo kama atabaki ndani ya Kagera Sugar ataendelea kubaki TPL.
Wewe ni mwenyeji na unazijuwa timu zote nje ndani uchague timu yenye maendeleo na malipo pamoja na marupurupu ya hakika na ujiepushe na migohoro ya kila siku
ReplyDeletesimba na Azam haziwezi kusajili wachezaji wote nakushauri nenda Yanga pamoja na matatizo yao unaweza pata namba na kuonekana kimataifa ukapate rizk huko nje
ReplyDeleteNenda Simba ukumbuke yote waliyoyapata wachezaji WA Simba ambao hawakuyapata wachezaji wowote WA timu nyengine bila yakutokea malumbano yoyote baina ya wachezaji na uongozi Kwa muda wote WA msimu.
ReplyDeleteNenda Simba ili Salamba asiwe pekeake! pili acha ujinga wa kuweka maslahi mbele (kwa mpira upi?) Maslahi yako mbele, huu ni muda wa kutengeneza mazingira yatakayokupeleka kwenye maslahi uyatakayo.
ReplyDeleteHahaha unataka asiweke maslahi basi ended Huko acheze bila ya maslahi na akiuliza afukuzwe. Mpira ndio uliowafanya akina Samata mamilionea na unamshsuri mtoto wawatu asiweke mbele masilaha
ReplyDelete