June 28, 2019



SELEMAN Ndikumana, mshambuliaji kutoka Al Adalah ya Saud Arabia amejiunga na klabu ya Azam FC kwa kuasini kandarasi ya mwaka mmoja.

Ndikumana raia wa Burundi ametua Azam FC baada ya kupendekezwa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije.

Hii ni timu ya pili kuwahi kucheza nchini Tanzania, nyingine ikiwa ni Simba aliyochezea 2006, pia akiwa na uzoefu barani Ulaya, akipita Molde ya Norway na FK Tirana ya Albania.

Huo ni usajili wa tatu kwa Azam FC, kwa ajili ya msimu ujao baada ya awali kulamilisha usajili wa wachezaji wengine wawili, winga Idd Seleman 'Nado' na kiungo mshambuliaji, Emmanuel Mvuyekure.

Kikosi cha Azam FC hivi sasa kipo kwenye maandalizi makali kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame, inayotarajia kuanza kutimua vumbi Julai 7 nchini Rwanda, ikiwa kama bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic