June 30, 2019


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kufunguliwa kwa Dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2019/2020.

Dirisha litafungwa Julai 31, 2019 na hakutakua na muda wa ziada.

Usajili wa mashindano ya CAF kwa klabu za Simba,Young Africans, Azam FC na KMC wenyewe utafungwa Julai 10, 2019.

Baada ya kipindi hicho cha usajili Klabu zitakua na siku tisa za kusajili kwa kulipa faini ya USD 250 Julai 11-Julai 20, 2019 kabla ya kipindi cha pili kitakachokua na siku 10 kuanzia Julai 21-Julai 31, 2019 kipindi ambacho watalipa USD 500 na mchezaji ataanza kutumika kuanzia raundi ya pili.

Simba na Young Africans wanawakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa wakati Azam FC na KMC wanawakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho.

TFF inasisitiza Klabu zote kufanya usajili kwa wakati.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic